Arsenal wamaliza vinara kundi lao UEFA

Lucas Perez scores Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lucas Perez alikuwa amefungia Arsenal magoli mawili pekee awali kabla ya 'hat-trick' hiyo Basel

Arsenal wamefanikiwa kuwaliza kileleni katika Kundi A Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya FC Basel ya Uswizi.

Ufanisi huo ulitokana na mabao matatu aliyoyafunga kiungo Lucas Perez na kuwawezesha kushinda 4-1.

Wapinzani wao Paris St-Germain, ambao kabla ya mechi za Jumanne walikuwa wanaongoza kundi, walishuka na kumaliza nambari mbili baada ya kutoka sare na Ludogorets Razgrad wa Bulgaria mjini Paris.

PSG wangefanikiwa kumaliza vinara iwapo wangeshinda mechi hiyo, lakini hilo halikuwa.

Perez alifungua Arsenal mabao matatu nalo la nne likatoka kwa Alex Iwobi kabla ya Seydou Doumbia kufungia Basel bao la kufutia machozi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kumaliza kileleni kundi lao tangu msimu wa 2011-12.

Hata hivyo, vijana hao wa Arsene Wenger hawakufanikiwa kusonga zaidi ya hatua ya 16 bora mwaka huo.

Wamekuwa wakiondolewa kwenye michuano hiyo hatua hiyo ya muondoano kila msimu kwa misimu sita iliyopita.

Kando na kufanikiwa kumaliza kileleni Gunners, pia wamefanikiwa kumaliza michuano ya hatua ya makundi bila kushindwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2005-06, msimu ambao walifika fainali.

Haki miliki ya picha BBC Sport

Gunners' good fortune?

Drooo ya hatua ya makundi itafanyika Jumatatu na Arsenal wamefanikiwa kuwakwepa Barcelona na Monaco, waliowaondoa kwenye michuano misimu miwili iliyopita. Aidha, wamewahepa pia Atletico Madrid na Napoli.

Hata hivyo, wanaweza kukutana na mmoja wa hawa:

  • Bayern Munich, waliowachapa 2013 na 2014
  • Borussia Dortmund au Real Madrid
  • Benfica
  • Bayer Leverkusen
  • Porto au FC Copenhagen
  • OJuventus, Seville au Lyon
Haki miliki ya picha AP
Image caption Kieran Gibbs pia aling'aa mechi hiyo
Watakaofuzu hatua ya Muondoano
Kundi A: PSG na Arsenal, Europa League (EL) - Ludogorets
Kundi B: Benfica na Napoli, EL - Besiktas
Kundi C: Barcelona na Manchester City, EL - Borussia Monchengladbach
Kundi D: Atletico Madrid na Bayern Munich, EL - FC Rostov
Kundi E: Monaco na Bayer Leverkusen
Kundi F: Borussia Dortmund na Real Madrid
Kundi G: Leicester na mmoja kati ya Porto na FC Copenhagen
Kundi H: Juventus na mmoja kati ya Sevilla na Lyon

Mada zinazohusiana