Kina dada wa Nigeria wakatalia hotelini Abuja

Mabingwa wa Afrika Nigeria Haki miliki ya picha Darius Meke

Wachezaji wa timu ya soka ya kina dada ya Nigeria wamekataa kuondoka hotelini mjini Abuja, kuishinikiza serikali kuwalipa bonasi na marupurupu waliyoahidiwa kwa kushinda Kombe la Taifa Bingwa Afrika upande wa Wanawake.

Super Falcons, ambao walishinda taji lao la nane la ubingwa Afrika mnamo Jumamosi kwa kuwalaza wenyeji Cameroon 1-0, wanalilalamikia shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kwa kukosa kulipa kila mchezaji dola za Kimarekani $17,150 kama walivyokuwa wameahidiwa.

Inadaiwa kwamba maafisa wa NFF walikuwa pia wameahidi kuwalipa wachezaji hao malimbikizi ya marupurupu waliyofaa kulipwa wakati wa mechi za kufuzu, pamoja na bonasi ya [dola za Kimarekani $6,500] kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Mmoja wa wachezaji aliambia BBC kwamba wataendelea kukaa katika hoteli ya Agura hadi walipwe pesa hizo ambazo zinafikia dola za Kimarekani $23,650 kwa kila mchezaji.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii