Fifa kuanza kutumia Video michezoni

fifa Haki miliki ya picha Google
Image caption Fifa kutumia video kusaidia waamuzi

Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu yanaanza Leo huko Japan na waamuzi wa Mechi hizo watapata msaada wa maamuzi yao kwa kutumia Video kutoka kwenye Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

Mfumo wa Video kusaidia maamuzi ya waamuzi wawapo Uwanjani umefanyiwa Majaribio rasmi ya FIFA kwa mara ya kwanza katika Mechi ya Kimataifa mwezi Septemba wakati Italy ilipocheza na Ufaransa huko Bari.

Kwenye Mfumo huo wa Video, mwamuzi Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

VARs imekuwa ikitumika kwa Majaribio huko Marekani kwenye Ligi Daraja la 3 na sasa FIFA, ikishirikiana na IFAB, ambacho ndicho chombo pekee kinachoweza kubadili Sheria za Soka, vimeafika Majaribio hayo na sasa yameingia hatua mpya .

Mashindano hayo yanaanza Leo huko Yokohama kwa Wenyeji Kashima Antlers kucheza na Auckland City ya New Zealand.