Europa League: Manchester United wafuzu hatua ya muondoano

Henrikh Mkhitaryan Haki miliki ya picha ProSports/REX/Shutterstock
Image caption Henrikh Mkhitaryan aliwahi kufunga mabao matatu uwanja wa Chornomorets akichezea Borussia Dortmund

Manchester United walilaza Zorya Luhansk na kufika hatua ya klabu 32 bora katika ligi ndogo ya Ulaya, Europa League, katika mechi ambayo Henrik Mkhitaryan aliwafungia bao la kwanza Alhamisi.

Red Devils walitawala mchezo huo uliochezewa Odessa nchini Ukraine na kuondoka na ushindi wa 2-0.

Makombora ya mbali kutoka kwa Wayne Rooney na Paul Pogba yalikuwa ya kuvutia zaidi, ingawa hawakufanikiwa kufunga.

Kipindi cha kwanza, walidhibiti mpira asilimia 76.

Mkhitaryan, ambaye sasa ameanza mechi tatu mtawalia, alikuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Sergio Romero alifanya kazi ya ziada na kuhakikisha wanasalia kifua mbele kabla ya Zlatan Ibrahimovic kufunga la pili.

United walifuzu wakiwa nyuma ya Fenerbahce, ambao walishinda 1-0 ugenini Feyenoord.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Paul Pogba alivuma kwenye mchezo huo na alipata mpira sana

Jose Mourinho wanapigiwa upatu kufana katika michuano hiyo kwa sasa, lakini kwa sababu walimaliza Kundi A wakiwa nambari mbili, watakuwa hawajawekwa kwenye kitengo chochote. Droo itafanyika Jumatatu.

Manchester United wanaweza kupewa
Washindi wa makundi Europa League: Apoel Nicosia, Saint-Etienne, Zenit Saint Petersburg, Roma, Athletic Bilbao, Ajax, Shakhtar Donetsk, Schalke, Fiorentina, Sparta Prague, Osmanlispor
Klabu zilizotoka Ligi ya Kbali Bingwa Ulaya: FC Copenhagen, Lyon, Besiktas

Manchester United, ambao wamo nambari sita Ligi ya Premia, watakutana na Tottenham Jumapili.

Mada zinazohusiana