Watford yainyamazisha Everton

Mshambuliaji wa Watford Okaka akifunga bao lake la kwanza kupitia kisigino
Image caption Mshambuliaji wa Watford Okaka akifunga bao lake la kwanza kupitia kisigino

Stefano Okaka aliifungia Watford mabao yake ya kwanza katika ligi ya Uingereza.

Okaka, aliyesajiliwa kutoka Anderlecht msimu uliopita,alifunga bao lake la kwanza kwa umaihiri mkubwa kabla ya kufunga bao lake la pili kufutia kona.

Sebastian Prodl alifunga bao la pili kwa upande wa Watford kupitia krosi iliopigwa na Jose Holebas

Everton ilikuwa ya kwanza kufunga kupitia mshambuliaji wake matata Romelu Lukaku kufuatia pasi iliopigwa na mchezaji Barry kabla ya kufunga bao la pili na la kufutia machozi katika dakika za mwisho za kipindi.