Chelsea wajikita kileleni kwa alama sita

Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wote waliifungia Man U
Image caption Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wote waliifungia Man U

Chelsea wameweka pengo la alama sita na kuendelea kubaki kileleni mwa ligi kuu soka England baada ya goli alilofunga kiungo Cesc Fabregas kipindi cha kwanza kuwa pekee na la ushindi.

Fabregas alipachika goli hilo kwa ufundi wa hali ya juu kwa kuupeleka mpira kwenye kona ya kushoto ya lango la Sunderland baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Willian na kuwa ushindi wa kumi mfululizo kwa Chelsea.

Image caption Cesc Fabregas amefunga magoli mengi dhidi ya Sunderland (matano) hii ikiwa ni zaidi ya timu yoyote kwenye EPL aliyokutana nayo

Ulikuwa ni ushindi muhimu sana kwa Chelsea baada ya Arsenal kuteleza siku ya Jumanne kwa kuchapwa 2-1 na Everton na hii inamaanisha vijana wa Antonio Conte watakuwa kileleni mwa ligi hiyo kwa msimu huu wa Christmas.

Matokeo ya michezo mingine

Middlesbrough 0-3 Liverpool

West Ham 1-0 Burnley

Crystal Palace 1-2 Manchester Utd

Manchester City 2-0 Watford

Stoke city 0-0 Southampton

Tottenham Hotspur 3-0 Hull City

West Bromwich Albion 3-1 Swansea City