Petra Kvitova ashambuliwa kwa kisu

Chekslovakia
Image caption Petra Kvitova

Bingwa wa zamani wa mchezo wa Tennis Wimbledon, Petra Kvitova, amefanyiwa upasuaji kwenye mkono wake kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa kisu katika moja ya miji ya Jamhuri ya Chekslovakia.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa kijamii , ameeleza kuwa alishtushwa na shambulizi hilo na anajiona ana bahati kuwa hai baada ya kujitetea mwenyewe dhidi ya shambulizi hilo.

Msemaji wa bingwa huyo wa zamani ambaye anapewa nafasi ya kumi na moja kwa ubora duniani kwenye mchezo wa tenisi, amesema kwamba, afya ya bingwa huyo itatengamaa baada ya miezi mitatu.

Petra Kvitova aliwahi kuwa bingwa mchezo wa tenisi wa Wimbledon mwaka wa 2011 na 2014.