Wenger: Nina kinga dhidi ya ukosoaji mbaya

Mashabiki wa Arsenal wanaomtaka Arsene Wenger kuondoka katika klabu hiyo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki wa Arsenal wanaomtaka Arsene Wenger kuondoka katika klabu hiyo

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ''amemea kinga'' dhidi ya ukosoaji wa kupita kiasi, wakati ambapo timu yake inalenga kuimarisha harakati zake za kushinda taji la ligi itakapokutana na West Brom Albion katika siku kuu ya Boxing Dei.

Gunners wako katika nafasi ya nne katika jedwali ,baada kushuka kwa alama tisa chini ya viongozi Chelsea kufuatia ushindi wao dhidi ya Everton na Manchester City.

Wenger akiwa katika msimu wake wa 20 na Arsenal alifananisha soka na jamii pamoja na siasa akisema kila mtu ana maoni yake.

Je, Arsenal imeanza kupoteza pumzi za kushinda taji? Raia huyo wa Ufaransa ,ambaye kandarasi yake inakamiika mwishowe wa msimu huu amesema kuwa anaendelea kujiuliza kila mara.

Image caption Arsene wenger anasema kuwa amemea kinga dhidi ya ukosoaji wa kupita mpaka

''Sina kinga dhidi ya ukosoaji'' ,aliongezea ''lakini ukosoaji wa kupita kiasi ndio''.

''Nimehudumu kwa muda mrefu kwa mimi kuhangaishwa na watu wanaopenda klabu hii ambao huwa wamekasirika sana ifikiapo Ijumatatu asbuhi lazima tuwaelewe.Haimanishi kwamba ahawatabadili msimamo wao tutakaposhinda mechi inayofuata''.