Maafisa wa Urusi wakiri kuwepo kwa udanganyifu

Urusi Haki miliki ya picha Getty Images

Kwa mara ya kwanza, Maafisa wa Urusi wamekiri kuwepo kwa mipango ya matumizi ya dawa zilizoharamishwa iliyoathiri mashindano makubwa duniani.

Ripoti iliyotolewa mnamo tarehe 9 Disemba, ilisema kuwa zaidi ya wanamichezo 1,000 wa Urusi walinufaika na udanganyifu kati ya mwaka wa 2011 na 2015.

Kwenye mahojiano na jarida la New York times, maafisa walikiri mpango huo lakini wakapinga kwamba ilidhaminiwa na serikali.

"Ilikuwa ni mikakati iliyopangwa," amesema Anna Antseliovich, kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka kuu ya kuchunguzi matumizi ya dawa za kusisimua misuli nchini Urusi