Chelsea yaifikia rekodi ya Arsenal ya ushindi

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte hatahivyo amesema kuwa lengo la Chelsea sio rekodi bali ni taji la Uingereza
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte hatahivyo amesema kuwa lengo la Chelsea sio rekodi bali ni taji la Uingereza

Chelsea imeshinda mechi yake ya 13 mfululizo katika mchuano wa ligi kuu ya Uingereza Premier League.

Sasa inawiana na rekodi kama hiyo ya Arsenal.

Wakiongozwa na meneja wao Antonio Conte Chelsea imeishinda Stoke City mabao manne kwa mawili huko Stamford Bridge.

Kwa hivyo ni sherehe mara mbili - mwaka mpya na pointi sita mbele ya nambari mbili ambao ni Liverpool, walioichara Manchester City bao la kufunga mwaka moja bila.

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte hatahivyo amesema kuwa lengo la Chelsea sio rekodi bali ni taji la Uingereza

Mada zinazohusiana