Wenger: Bao la Giroud miongoni mwa 5 bora

Bao la Giroud dhidi ya Crystal Palace Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bao la Giroud dhidi ya Crystal Palace

Bao la Olivier Giroud la 'scorpion ama nge' katika ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace ni miongoni mwa mabao matano muhimu katika uongozi wa Arsene Wenger.

Mabao ya Thiery Henry na Dennis Bergkamp ni miongoni mwa mbao aliyofurahia lakini akasema hili litakuwa 'bao la Giroud'.

Aliongezea: Si bao la kawaida lakini Giroud's alitoa kitu maalum.

Giroud amesema kuwa bao hilo alilifunga kwa bahati.

Uvamizi wa Arsenal katika ngome ya Crystal Palace ulimfanya Giroud kufunga bao hilo maridadi kutoka kwa krosi iliopigwa na Alexi Sanchez.