Jose Mourinho achukizwa na Ivory Coast

Beki wa Manchester United Eric Bailey akizungumza na kocha Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa Manchester United Eric Bailey akizungumza na kocha Jose Mourinho

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amechukizwa na Ivory Coast baada ya kumchukua beki Eric Bailey

Bailey alishiriki katika kikosi cha kwanza cha United katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Middlesbrough na Mourinho alidhani beki huyo atajuimuika na wenzake katika mechi dhidi ya West Ham siku ya Jumatatu.

Mourinho ameambia mtandao wa klabu hiyo kwamba kocha Michel Dussuyuer alikuwa hayuko tayari kuchukua hatari yoyote wakati wanapijiandaa kutetea taji lao la Afrika.

''Baily anaondoka anaenda kuchezea timu yake ya taifa,alisema Mourinho.Ni lazima awe na timu yake mnamo tarehe 2 Januari.Tuliwaomba wamchukue tarehe 3 lakini wakakataa,kwa hivyo hawezi kucheza dhidi ya West Ham''.