Afcon 2017: El Hadary kuweka rekodi soka ya Afrika

Veteran goalkeeper Essam El Hadary Haki miliki ya picha MOHAMED EL-SHAHED

Golikipa mkongwe wa Misri Essam El Hadary huenda akaibuka mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kucheza katika fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika baada yake kutajwa kwenye kikosi kitakachowakilisha taifa hilo Gabon.

El Hadary anatimiza miaka 43 mwezi huu na yumo kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Misri watakaosakata gozi Gabon.

Rekodi ya sasa inashikiliwa na Mmisri mwingine Hossam Hassan aliyecheza mwaka 2006 akiwa na miaka 39.

Kocha wa timu ya taifa Hector Cuper aliwaondoa wachezaji wanne kutoka kwenye kikosi shikilizi na kusalia na kikosi chake cha mwisho.

Waliotemwa na beki Hamada Tolba na kiungo wa kati Ahmed Gomaa wa Al Masry, kiungo wa kati wa Zamalek Mohamed Ibrahim na kipa wa Ismaili Mohamed Awad.

Babu atafuta klabu mpya ya kuchezea

Ni wachezaji wanne pekee wa kikosi cha Misri kilichocheza fainali za mwisho walizoshiriki mwaka 2010 ambapo walifanikiwa kutwaa kombe hilo mara ya tatu mtawalia.

Wachezaji hao ni El Hadary, Ahmed Elmohamady, Mohamed Abdelshafi na Ahmed Fathi.

Misri, ambao walikosa fainali tatu zilizopita, wamo Kundi D ambapo watafungua kampeni yao dhidi ya Mali mnamo tarehe 17 Januari dhidi ya Mali.

Michuano hiyo itachezewa Gabon 14 Januari hadi 5 Februari.

Kikosi cha Misri:

Walinda lango: Sherif Ekramy (Al Ahly), Essam El Hadary (WadiDegla), Ahmed El Shennawi (Zamalek)

Mabeki: Mohamed Abdelshafi (Al Ahly Jeddah), Ahmed Dwidar(Zamalek), Ahmed Elmohamady (Hull City), Ahmed Fathi (Ahly),Omar Gaber (FC Basle), Ali Gabr (Zamalek), Karim Hafez (RacingLens), Ahmed Hegazy, Saad Samir (both Al Ahly)

Viungo wa kati: Mohamed Elneny (Arsenal), Abdallah El Said (AlAhly), Mahmoud Trezeguet Hassan (Royal Mouscron-Peruwelz), TarekHamed, Ibrahim Salah (both Zamalek), Amr Warda (Panetolikos)

Washambuliaji: Mahmoud Abdelmoneim Kahraba (Al Ahly Jeddah),Ahmed Hassan Kouka (Sporting Braga), Marwan Mohsen (Al Ahly),Mohamed Salah (Roma), Ramadan Sobhi (Stoke City).

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii