John Obi Mikel aihama Chelsea na kwenda China

Chelsea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mikel ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League akiwa na Chelsea

Kiungo wa kati wa Nigeria John Obi Mikel amekuwa mchezaji wa karibuni zaidi kuondoka Chelsea na kuhamia Ligi Kuu ya China.

Mikel ametangaza kwenye Twitter kwamba atajiunga na klabu ya Tianjin TEDA.

Majuzi, Oscar aliondoka Stamford Bridge na kujiunga na Shanghai SIPG.

Mchezaji wa Brazil Ramires alikuwa ameaga klabu hiyo mwaka jana.

Mikel, ambaye amekaa miaka 10 Chelsea, hajapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza msimu huu chini ya meneja wa sasa Antonio Conte.

Haki miliki ya picha Getty Images

Amesema kwenye taarifa: "Kama mnavyofahamu, sijacheza sana msimu huu kama ambavyo ningelipenda, na ikizingatiwa kwamba nina miaka 29, nina miaka mingi sana ya kucheza."

Taarifa za habari zinasema amehama kutoka London bila kulipiwa pesa zozote na atakuwa akilipwa takriban pauni 140,000 ($173,432) kila wiki.

Mada zinazohusiana