Mourinho aionya Liverpool siku ya Jumapili

Mourinho ameionya Liverpool kwamba mechi ya Jumapili haitakuwa matembezi ya mbugani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mourinho ameionya Liverpool kwamba mechi ya Jumapili haitakuwa matembezi ya ukumbi wa filamu

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wake kwamba mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool haitakuwa ''matembezi ya ukumbi wa filamu' na badala yake ameitaka Liverpool kujiandaa vilivyo.

United iliishinda Hull City 2-0 katika awamu ya kwanza ya mechi ya kombe la Ligi EFL siku ya Jumapili kufuatia mabao ya Juan Mata na Marouane Fellaini yaliotikisa wavu.

Hatahivyo Mourinho amesema kuwa kila mchezaji anafaa kufanya kazi ya ziada dhidi ya Liverpool.

''Ni mechi muhimu sana kwetu, alisema.Tunapocheza vyema mashabiki pia hushirikiana nasi .

Tunaposhndwa kucheza vizuri ni vyema kwamba mashabiki hawapaswi kulalamika sana.

Kila mtu anapenda mechi kubwa, wachezaji,wakufunzi na mashabiki. Kila mmoja anapenda mechi kubwa kwa hivyo tuelekee katika mechi hiyo siku ya Jumapili''.

Liverpool imepoteza mara mbili pekee msimu huu ,ikiwa imeshindwa 4-3 na Bournemouth mnamo tarehe 4 mwezi Disemba.

Timu hiyo ya Jurgen Klopp ni ya pili katika ligi ya Uingereza, ikiwa pointi tano mbele ya United iliopo katika nafasi ya sita na pointi tano nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea.