Dimitri Payet akataa kuichezea West Ham

Mshambuliaji wa West Ham Dimitri Payet Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa West Ham Dimitri Payet

Mkufunzi wa klabu ya West Ham Slaven Bilic amesema kuwa mshambuliaji Dimitri Payet hataki tena kuichezea West Ham , lakini klabu hiyo haiko tayari kumuuza.

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na swala la kuihama timu hiyo.

''Tumesema kuwa hatuwezi kuwauza wachezaji wetu wazuri lakini Payet hataki kutuchezea tena'', alisema Bilic.

''Hatuwezi kumuuza''. Payet alijiunga na West Ham kutoka Merseille kwa kitita cha pauni milioni 10.7 mnamo mwezi Juni 2015.

Alifanikiwa katika msimu wa kwanza na klabu hiyo ,akifunga mabao 12 na kuteuliwa miongoni mwa uzo la wachezaji bora la kila mwaka.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa West Ham Slaven Bilic na mshambuliaji wake Dimitri Payet

Ijapokuwa amefunga mara tano msimu huu, Payet ameshindwa kufikia kiwango kama hicho na gazeti la The Sun liliripoti wiki ilioipita kwamba Bilic alimuagiza mchezaji huyo kubadili tabia yake.

Aliwachwa nje katika mechi ya FA siku ya Ijumaa ambapo West Ham ililazwa 5-0 na Manchester City.

West Ham iko nafasi ya 13 katika ligi ya Uingereza, alama saba juu ya eneo la kushushwa daraja na sasa itakwaruzana na Crystal Palace siku ya Jumamosi.