Claudio Makelele ndiye msaidizi wa kocha Swansea

Claudio Makele kuwa naibu wa kocha Swansea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Claudio Makele kuwa naibu wa kocha Swansea

Klabu ya Swansea City imemsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Ufaransa na Chelsea Claudio Makelele kuwa naibu wa kocha.

Makelele mwenye umri wa miaka 43 amesaini kandarasi hadi mwisho wa msimu.

Makelele anajiunga tena na kocha Paul Clement ambaye alifanya kazi naye akiwa mchezaji wa Chelsea kutoka mwaka 2007-2008 pamoja na akiwa mkufunzi wa PSG chini ya meneja Carlo Ancelotti.

''Nimefurahi sana kuwa hapa na kufanya kazi na Swansea, alisema Makelele.Paul ni mshauri wangu .Amenifunza mengi wakati nilipofanya kazi naye.Niliposikia kwamba alirudi katika ligi ya Uingereza nilimpigia simu na kumuuliza iwapo naweza kumsaidia kaklabu ya Swansea''.

Makelele atakuwa katika mechi ya Swansea dhidi ya Arsenal