Everton yaishinda Man City mabao 4-0

Romelu Lukaku aliifungua Everton bao la kwanza dakika ya 33 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Romelu Lukaku aliifungua Everton bao la kwanza dakika ya 33

Everton imonyesha mchezo mzuri kwa kuipa kichapo Man City mabao 4-0, ambalo ni pigo kubwa kwa meneja wa City Pep Guardiola.

Romelu Lukakku aliifungia Everton bao la kwanza mnano dakika ya 33 alipopata pasi safi kutoka kwa Kevin Mirallas.

Dakika mbili baada ya kuunza kwa kipindi cha pili, Kevin Mirallas alitumia fursa ya safu duni ya ulinzi ya Man City na kupenyeza mpira langoni.

Tom Davies aliifungia Everton bao la tatu mnamo dakika ya 79, naye Ademola Lookman akifunga bao la nne wakati zikitimia dakika nne za ziada.

Evertona inapata ushindi huo baada ya kipigo cha Leicester wiki iliyopita.