Mtanzania Felix Simbu ashinda Marathon India
Huwezi kusikiliza tena

Mtanzania Alphonce Felix Simbu ashinda Marathon India

Mwanariadha wa Tanzania Felix Alphonce Simbu Jumapili alishinda nafasi ya kwanza katika mashindano ya mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon.

Simu alimaliza mbio hizo kwa muda wa 2:09:32 kuzawadiwa dola za Kimarekani 42,000.

Mkenya Joshua Kipkorir alimaliza wa pili kwa muda wa 2:09:50, naye Mkenya mwenzake Eliud Barngetuny akamaliza wa tatu na muda wa 2:10:39.

Mkenya Bornes Kitur alishinda mbio hizo upande wa wanawake.

Simbu alizungumza na Shedrack Mwansasu kwa njia ya simu kutoka Mumbai.

Mada zinazohusiana