Bacary Sagna atozwa faini ya £40,000

Bacary Sagna Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bacary Sagna

Beki wa Manchester City Bacary Sagna, ametozwa faini ya pauni elfu 40 na shirikisho la soka nchini Uingereza FA baada ya kuchapisha '10 dhidi 12'' katika mtandao wake wa Instagram kufuatia mechi kati yao na Burnley.

Beki huyo wa kimataifa mwenye umri wa miaka 33 kutoka Ufaransa alisema hayo wakati timu yake ilipopata ushindi wa mabao 2-1 katika ligi ya Uingereza Januari 2.

City walipunguzwa na kusalia wachezaji 10 katika dakika ya 32 ya mchezo , pale mwamuzi Lee Mason alipomtoa nje kiungo wa kati Fernandinho.

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limesema katika taarifa , ambayo ilifutwa kwamba chapisho hilo lilihoji uadilifu wa mechi hiyo.

Sagna pia ameonywa kuhusu mwenendo wake.

City hatahivyo haijaondoa uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya faini hiyo.