Djokovic atolewa michuano ya Australian open

Mara ya mwisho Djokovic kupoteza katika mzunguko wa pili ilikuwa 2008
Image caption Mara ya mwisho Djokovic kupoteza katika mzunguko wa pili ilikuwa 2008

Bingwa mtetezi Novak Djokovic amewashangaza wengi baada ya kuchapwa na mchezaji namba 117 duniani Denis Istomin raia wa Uzbektan katika michuano ya Australian Open.

Mshindi huyo mara sita wa michuano hiyo ameshindwa kwa seti 7-6 5-7 7-6 6-4.

Katika matokeo mchezaji Andy Murray amesalia katika nafasi ya kwanza kushinda tuzo ya Australian open huko mjini Melbourne.

Briton Murray, ambaye amefikia katika nafasi ya tatu amepoteza katika fainali tano kwa miaka saba iliyopita mjini Melbourne, nne kati ya hizi kwa Djokovic.

Hii ni mara ya pili pekee katika miaka saba ambapo Djokovic kupoteza ushindi kwa mchezaji aliyeko kati ya wachezaji 100 kushindwa kwake na Juan Martin del Potro aliyekuwa katika nafasi ya 145 katika mashindano ya olimpiki yaliyofanyika huko Rio mwaka 2016.

Uzbek Istomin atapambana na mhispania Pablo Carreno Busta, aliyemshinda Muingereza Kyle Edmund ifikapo Alhamisi.