Manchester United: Memphis Depay ahamia Lyon

Manchester United winger Memphis Depay celebrates scoring a goal Haki miliki ya picha Rex Features

Manchester United wamemuuza Memphis Depay kwa klabu ya Ufaransa ya Lyon kwa ada inayokadiriwa kufikia £16m.

Ada yake huenda ikafikia £21.7m, ukiongeza marupurupu yatakayotegemea miongoni mwa mengine iwapo Lyon watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Depay kupata mkataba mpya.

United pia wameweka kifungu cha kuwawezesha kumnunua mchezaji huyo tena iwapo watamhitaji.

Aidha, watakuwa na usemu kuhusu kuuzwa kwake.

Depay, 22, amefunga mabao saba katika mechi 53 alizocheza tangu kujiunga na United kwa £31m kutoka PSV Eindhoven Mei 2015.

Ada yake ya awali ilikuwa £25m.

Makubaliano ya Man Utd na PSV yalikuwa pia na masharti ya malipo ya ziada ambayo hayajatimizwa.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Memphis Depay baada ya kuwafunga Watford Novemba 2015

Msimu huu, Mholanzi huyo amechezea United mechi nane pekee, lakini amechezeshwa dakika nane pekee tangu mwisho wa Oktoba.

Jose Mourinho anasema hilo limetokana na ushindani mkubwa Old Trafford.

Mada zinazohusiana