Ivory Coast na DRC watoka sare ya mabao 2-2

Ivory Coast wakisherehekea bao lao la kwanza Haki miliki ya picha ISSOUF SANOGO
Image caption Ivory Coast wakisherehekea bao lao la kwanza

Mabingwa Ivory Coast walijikakamua na kutoka sare ya mabao mawili na DRC na kufufua matumaini yao ya kufika robo fainali ya kombe la taifa bingwa barani Afrika.

DRC ndiyo iliona lango kwanza kupitia mpira uliorushwa na Neesken Kebano lakini bao hilo lilisawazishwa baadaye na Wilfired Bony aliyefunga kwa njia ya kichwa.

DRC tena ilifanikiwa kufunga bao la pili dakika mbili baada ya Ivory Coast kusawazisha kupitia kwa Junior Kabananga.

Ivory Coast bila kusita kwa mara nyingine walisawazisha bao hilo kupitia mkwaju mzito wa Serey Die.