West Ham yamsaini nahodha wa Southampton Jose Fonte

Fonte aliichezea Southampton mara 286 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fonte aliichezea Southampton mara 286

West Ham imemsajili nahodha wa Southampton Jose Fonte kwa kima cha pauni milioni 8 kwa mkataba wa miaka miwili unusu.

Fonte raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliichezea Southampton kwa miaka saba, aliomba kuihamia West Ham ikiwa imesalia miezi 18 kabla ya mkataba wake kumalizika.

Mkurugenzi wa Southampton Les Reed anasema kuwa Fonte alikuwa na fursa ya kusaini mkataba bora lakini akaomba kuondoka.

Fonte amesema kuwa meneja wa West Ham Slaven Bilic alichangia pakubwa kumshawishi kuichagua West Ham.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea