Saido Berahino: Stoke wakamilisha kumnunua mshambuliaji wa West Brom

Berahino Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Saido Berahino alichezea West Brom mara ya mwisho 10 Septemba dhidi ya Bournemouth

Klabu ya Stoke City imekamilisha kumnunua mshambuiaji wa West Brom Saido Berahino kwa ada ya £12m.

Ametia saini mkataba wa miaka mitano unusu.

Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 23 katika klabu ya West Brom ulitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu, lakini West Brom walimuahidi mkataba mwingine kwa mara ya tatu mwezi Desemba.

Mchezaji huyo hajacheza tangu Septemba na uhusiano wake na klabu hiyo umezorota tangu msimu wa 2014-2015.

Amesema amekuwa na miaka miwili migumu lakini sasa anafurahia kwamba yote yameisha na yuko tayari kurejea uwanjani.

Berahino alikasirishwa na hatua ya klabu yake kukataa ofa kutoka kwa Tottenham siku ya mwisho ya kuhama wachezaji majira ya joto 2015.

Miezi miwili baadaye, aliandika kwenye Twitter kwamba hangechezea West Brom tena wakiwa chini ya mwenyekiti wa wakati huo Jeremy Peace.

Januari 2015, alifunga mabao manne laini hakusherehekea, ishara ya kuonesha kutoridhika kwake katika klabu hiyo.

Mada zinazohusiana