Manchester City: Pep Guardiola asema huenda hajatosha

Pep Guardiola Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Guardiola ameshinda mataji ya ligi mara sita misimu saba aliyokuwa meneja Uhispania na Ujerumani

Pep Guardiola amesema huenda yeye ni mzuri vya kutosha kuwafaa wachezaji wa Manchester City, badala ya kuwa kwamba wachezaji ndio hawatoshi.

City wameshindwa mechi nne kati ya nane walizocheza karibuni Ligi ya Premia.

Walishuka hadi nambari tano kwenye jedwali baada ya kulazwa 4-0 na Everton Jumapili.

Watakutana na Tottenham nyumbani Jumamosi na Guardiola anasema maswali sasa yanafaa kuulizwa kumhusu yeye pamoja na kikosi chake.

"Sielewi huku kuwakosea heshima wachezaji wazuri, pale watu wanasema wachezaji hawa hawastahiki kuwa nami," alisema Mhispania huyo.

"Labda matarajio kuhusu kuja kwangu hasa na sifa tulizolimbikiziwa baada ya kushinda mechi 10 mtawalia labda zilitiwa chumvi kiasi,2 ameongeza.

"Huenda mimi si mzuri kiasi cha kuwafaa."

Haki miliki ya picha Opta

Baada ya kuanza kwa kishindo na kushinda mechi 10 mtawalia, meneja huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich anakubali kwamba hajazoea kuwa katika hali ambayo amejipata sasa.

Katika misimu saba aliyokuwa meneja wa klabu katika ligi kuu Uhispania na Ujarumani, alishinda mataji sita ya ligi, vikombe vinne vya ligi na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili.

"Ni mara yangu ya kwanza kujipata katika hali hii na nataka kukabiliana nayo, na sitasema kwamba wachezaji wangu si wazuri," alisema.

"Ninataka tuongoze ligi, lakini kwa sasa hatupo kileleni."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii