Balotelli abaguliwa nchini Ufaransa

Mshambuliaji wa NIce Mario Balotelli Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa NIce Mario Balotelli

Mshambuliaji wa klabu ya Nice nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia.

Mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 alichapisha katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua?

''Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa''.

Balotelli alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kuhudumia marufuku katika mechi iliotoka sare ya 1-1 huko Corsica.

Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo.

Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote.

Balotelli amefunga mabao 10 katika mechi 15 tangu kujiunga na Nice katika uhamisho huru kutoka Liverpool mwezi Agosti ,miaka miwili baada ya uhamisho wa pauni milioni 16 kuelekea Anfield.