Deulofeu ajiunga na AC Milan kwa mkopo

Gerard Deulofeu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gerard Deulofeu

Winga wa Everton Gerard Deulofeu, amejiunga na klabu ya Italia ya AC Milan kwa mkopo hadi msimu huu ukamilike.

Winga huyu wa miaka 22 ameshiriki mechi 13 na klabu ya Everton msimu huu.

Meneja wa Everton Ronald Koeman, wiki iliyopita alisema ameruhusiwa kuiaga klabu hiyo 'ili apate nafasi ya kucheza'.

Raia huyo kutoka Uhispania alijiunga na Everton kwa mkopo kutoka Barcelona msimu wa 2013-14 , na kuihama klabu hiyo kabisa mwaka wa 2015 kwa kitita cha pauni milioni 4.3.

Milan alitangaza uhamisho wake mara ya kwanza kupitia akaunti yake ya Twitter siku ya Ijumaa, lakini ujumbe huo ukafutwa haraka.

Mada zinazohusiana