Kiongozi wa magari ya Langalanga ya Formula one afutwa kazi

Bernie Ecclestone Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bernie Ecclestone

Bernie Ecclestone, ametolewa katika nafasi yake ya yakudhibiti mashindano ya magari ya langalanga ya Formula 1, baada ya Shirika la habari la Liberty la Marekani kukamilisha mkataba wake wa dola bilioni 8 ya kuumiliki mchezo huo.

Ecclestone,86, ambaye amesimamia mashindano hayo kwa zaidi ya miaka 40, ameteuliwa kama mwenyekiti mstaafu na atafanya kazi ya mshauri katika bodi hiyo.

Chase Carey, atahudumu katika nafasi ya Ecclestone ya mtendaji mkuu na kuongezea katika majukumu ya kuwa mwenyekiti

Liberty pia imemnunua meneja wa zamani wa magari ya Mercedes, Ross Brawn kwa mashindano ya F1.

Mkurugenzi wa ufundi wa zamani wa Ferrari ambaye alikuwa akifanya kazi kwa niaba ya mshauri wa Liberty ameteuliwa kuongoza kazi za ufundi katika kampuni ya mashindano ya F1.

Ecclestone, alisema mapema Jumatatu kwamba amelazimishwa ''kuondoka''

Aliiambia shirika la magari la Ujerumani la Auto Motor und Sport: '' Nilitolewa. Hii ni rasmi. Sitaongoza kampuni hiyo tena. Nafasi yangu imechukuliwa na Chase Carey''

Ecclestone, aliongeza kwamba hafahamu jukumu lake jipya linamaana gani, na akasita kuzungumzia swala hilo alipoulizwa na BBC Sport, walitangaza siku ya Jumapili kwamba atawacha wadfa wake wiki hii.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Magari ya langalanga

Liberty ilianza kutaka kumiliki mashindano hayo ya magari ya langalanga mwezi Septemba.

Mapema Januari wakakamilisha masharti mawili ya kisheria yaliokuwa yamesalia.

Mpango huo ulikamilika siku ya Jumatatu na shirika la habari la Liberty linatarajiwa kubadilisha jina lake na kutumia jina la kundi la Formula 1.

Pia Brawn, afisa mkuu wa ESPN Sean Bratches ameteuliwa kuhusika na maswala ya kibiashara.

Brawn na Bratches watakuwa chini ya Carey, mwenyekiti wa kampuni ya 21st Century Fox,