Sunderland yamsajili Lescott wa Aston Villa

Joleon Lescott Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joleon Lescott alishiriki mechi 30 na Aston Villa msimu uliopita

Klabu ya Sunderland imemsaini beki wa zamani wa Aston Villa Joleon Lescott kwa mkataba wa muda mfupi.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 34 , ambaye alikuwa akicheza chini ya meneja wa The Black Cats David Moyes huko Everton kati ya mwaka 2006 na 2009, amejiunga na klabu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu.

Lescott, aliiaga Aston Villa majira ya mwisho baada ya kushiriki msimu mmoja kwa klabu hiyo.

Baadaye alijiunga na AEK Athens, na kushiriki mechi nne na klabu hiyo ya Ugiriki kabla ya kupata jeraha na mkataba wake kufutiliwa mbali mwezi Novemba.

Sunderland iko katika nafasi ya mwisho katika jedwali la ligi ya Premia , wakiwa na alama 15, alama tatu juu timu zilizo hatarini kushushwa daraja.