Alex Ferguson: Manchester United wanaimarika chini ya Mourinho

Sir Alex Ferguson Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sir Alex Ferguson

Manchester United wanaendelea kuimarika chini ya meneja Jose Mourinho na 'ni bahati tu wamekosa' lakini wangekuwa wakikabiliana vilivyo na Chelsea, amesema meneja wa zamani Sir Alex Ferguson.

Ferguson,75, alistaafu kama meneja mwaka 2013, lakini bado ana uhusiano wa karibu na klabu hiyo Old Trafford kwani huhudhuria michezo yao mingi.

"Nafikiri Mourinho amefanya kazi kubwa,'' amesema Ferguson katika mahojiano na BBC Sports.

Ferguson pia alielezea kwa nini rekodi ya ufungaji magoli ya mshambuliaji wa Manchester united Wayne rooney haitavunjwa na mchezaji yoyote yule karibuni.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Manchester United Jose Mourinho

Jose Mourinho ni meneja wa tatu kuiongoza klabu ya Manchester United tangu Ferguson kustaafu, alipochukua nafasi ya Louis van Gaal mwezi Mei.

Ingawa Mourinho alishinda mechi tatu zake za kwanza akiwa na Manchester United, alishinda alama sita pekee kutoka kwa mechi saba za Ligi ya Premia zilizofuata.

Mada zinazohusiana