Leicester wamuuza beki wao Luis Hernandez Uhispania

Luis Hernandez Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hernandez alionekana mara ya mwisho walipokuwa wakikabiliana na Bournemouth

Leicester City wamemuuza Luis Hernandez kwa klabu ya Malaga kwa ada isiyojulikana, miezi sita baada ya kumsaini difenda huyo.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27, alishiriki mechi nane baada ya kujiunga na mabingwa hao wa Ligi ya Premia kutoka Sporting Gijon mwezi Julai

Amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na klabu ya Malaga, ambao wamo katika nafasi ya 14 katika ligi ya Uhispania.

Mechi yake ya mwisho kuwachezea Leicester ni walipokabiliana na Bournemouth tarehe 13 mwezi Disemba mwaka jana walipopata ushindi wa 1-0.

Mada zinazohusiana