Japan yapata bingwa wa kwanza wa sumo kwa miaka 19

Japan yapata bingwa wa kwanza wa sumo baada ya miaka 19 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Japan yapata bingwa wa kwanza wa sumo baada ya miaka 19

Japan imemtaja rasmi mwanamiereka wake kuwa bingwa wa dunia wa uzani mzito kwa miongo miwili, kama njia ya kuimarisha mchezo wa miereka ya kitamaduni.

Kisenosato, mwenye umri wa 30, alipandishwa cheo kuwa yokozuna wa hali ya juu baada ya kushinda katika shindano lake la kwanza la mwaka

Ni Mjapan wa kwanza kuwa mwanamiereka tangu Wakanohana mwaka 1998.

Wanamiereka watano kutoka Marekani, Samoa na Mongolia wamejiunga kwa muda mfupi.

Wanamiereka kutoka nchi za nje wameudhibiti mchezo huo wa sumo , na kusababisha wanamiereka wa kawaida kukosekana.

Kisenosato, ambaye ametoka Ibaraki kasakazini mwa Tokyo mwenye uzani 178kg ameorodheshwa wa pili tangu mwaka 2012.

Baada ya kuwa katika nafasi ya pili kwa mara kadhaa, hatimaye alipata ushindi katika shindano lake la kwanza , na kusababisha kupandishwa cheo kuwa Yokozuna katika shindano la mwaka 2017.

''Nakubali, na ubinadamu wangu,''kisenosato amesema alipokuwa akiwahutubia wanahabari baada ya shirikisho la wanamiereka la Sumo kumuidhinisha.

''Nitajitolea kwa jukumu hilo na sitailetea aibu jina la Yokozuna''

Mashabiki wa Japan watajivunia kuwaona wanamiereka kurudi uwanjani katika mchezo huo licha ya tamaduni yao.

Watatu hao wanatoka Mongolia, kufuatia nyayo za Asashoryu, ambaye ni yokozuna wa kwanza aliyetoka Mongolia mwaka 2003.

Walioshinda miereka kutoka Japan walikuwa ndugu Takanohana na Wakanohana ambao walimfikia Yokozuna mwaka 1994 na 1998 mtawalio.

Kwa miaka ya hivi majuzi , imeshuhudia idadi ya wanamiereka kutoka Japan imepungua, kwa sababu mchezo huo umeonekana kuwa mgumu ,na unaodhibiti maisha kwa kiasi kikubwa.

Wanamiereka chipukizi wa sumo hufanya mazoezi katika 'mabanda' ambapo hula , hulala na kufanya mazoezi kwa pamoja na wakati kujiweka katika hali kwani wanaamini itawaongezea