Real Madrid wabanduliwa Copa Del Rey

Wachezaji wa klabu ya Celta Vigo wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Real Madrid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa klabu ya Celta Vigo wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Real Madrid

Klabu ya ligi ya La Liga Celta Vigo imewalaza viongozi wa ligi hiyo Real Madrid na kufika katika nusu fainali ya kombe la Copa del Rey baada ya kutoka sare ya 2-2 na hivyobasi kufuzu kwa jumla ya mabao 4-3.

Wenyeji Celta Vigo ndio waliokuwa wa kwanza kucheka na wavu baada ya muda wa kupumzika kupitia beki Danilo aliyejifunga.

Christiano Ronaldo hatahivyo aliwasawazishia wageni baada ya kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya Daniel Wass kuiweka kifua mbele Celta Vigo.

Lucas Vazquez alifunga bao la pili kwa kichwa lakini halikuisaidia Real Madrid.

Msururu wa matokeo mazuri ya kutofungwa kwa upande wa klabu ya Real Madrid ulisitishwa na Sevilla mapema mwezi Januari.

Wameshinda mara moja katika mechi zao tano katika mashindano yote.