Serena Williams amshinda Venus na kushinda taji la Grand Slam

Serena Williams amemshinda dadaake mkubwa Venus Williams ili kushinda taji lake la saba la Australia Open Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serena Williams amemshinda dadaake mkubwa Venus Williams ili kushinda taji lake la saba la Australia Open

Serena Williams amemshinda dadaake mkubwa Venus Williams ili kushinda taji lake la saba la Australia Open na kuweka rekodi ya Opera kwa kushinda mataji 23 ya Grand Slam.

Serena mwenye umri wa miaka 35 alishinda katika seti za 6-4, 6-4 ili kumpiku Steffi Graf katika orodha ya washindi wakuu tangu Grand Slam kuwakubali wachezaji wa kulipwa 1968.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serena Williams baada ya kumshinda dadake mkubwa Venus Williams

Raia huyo wa Marekani sasa ataorodheshwa wa kwanza duniani kwa kumpiku aliekuwa mchezaji nambari moja upande wa wanawake Angelique Kebber kutoka Ujerumani.

Raia wa Australia Margeret Court ndiye mchezaji wa pekee ambaye yuko mbele ya Serena baada ya kushinda mataji 24 ya Grand Slam .