Real Betis watoka sare ya 1-1 na Barcelona

La Liga haina teknolojia ya goli Haki miliki ya picha Reuters
Image caption La Liga haina teknolojia ya goli

Bao la Luis Suarez dakika ya mwisho liliokoa jahazi la Barcelona na kusababisha kutoka sare ya bao moja na Real Betis.

Real Betis ilitawala mechi na mchango wao Dani Ceballos na Ruben Castro ukazaa matunda wakati Alex Alegria alipoutumbukiza mpira kwenye wavu.

Awali bao na Barcelona lilikataliwa kutokana kutokuwepo kwa teknolojia ya kutambua bao likivuka mstari wa goli kwenye michuano ya La Liga.

Hata hivyo Suarez alitumia fursa ya kipekee baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Lionel Messi dakika ya mwisho na kusawazisha .

Barcelona wako pointi moja nyuma ya Real Madrid ambao wana mechi mbili za kucheza ikiwemo ya nyumbani dhidi ya Real Sociedal siku ya Jumapili.