Mohamed Elneny nje michuano ya AFCON

Misri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mohamed Elneny kiungo wa kati wa timu ya Arsenal

Kiungo wa kati wa timu ya Arsenal Mohamed Elneny anakabiliwa na jukumu la kuhakikisha ana kuwa sawa kiafya ili kushiriki katika fainali za michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu AFCON, endapo nchi ya Misri itafanikiwa kufika hatua hiyo.

Elneny ni miongoni mwa wachezaji wakali wa Misri na tayari amekumbwa na tatizo la kifua wakati wa mchezo wa nusu fainali wakati timu yake ilipomenyana na Morocco.

Meneja wa timu timu ya Misri Ihab Lehata amethibitisha kuwa Elneny huenda asiingie uwanjani tena katika michuano hiyo.