'Wachezaji wangemsikiza Bob Marley'

Nyom ni miongoni mwa wachezaji waliokataa kuichezea Cameroon Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyom ni miongoni mwa wachezaji waliokataa kuichezea Cameroon

Wachezaji kadhaa wa taifa la Cameroon watatazama mechi ya fainali ya siku ya jumapili ya kombe la bara Afrika kwa majuto.

Takriban wachezaji wanane kutoka Cameroon walikataa kukubali mwaliko wa kuliwakilisha taifa lao nchini Gabon.

Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Senegal El Hadji Diouf ameambia BBC kwamba wachezaji hao wangemsikiliza msanii wa muziki wa Reggae Bob Marley.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bob Marley

''Sielewi watu wanaokataa kuwakilisha mataifa yao'', mshambuliaji huyo wa Senegal aliambia tovuti ya BBC.

''Na alivyosema Bob Marley iwapo hujui unakotoka hujui kwa kwenda'',alisema.