Leo ni fainali kati ya Cameroon na Misri

Cameroon wamewashinda Senegal na Ghana kufika fainali Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cameroon wamewashinda Senegal na Ghana kufika fainali

Misri itajaribu kushinda kombe la taifa bingwa barani Afrika hii leo wakati wakikutana na Cameroon katika fainali.

Misri ni moja ya timu bora zaidi katika mechi zinazoandaliwa nchini Gabon na ndio washindi wa mwaka 2006,2008 na 2010 kaba ya kushindwa kufuzu kwa mashindano ya mwaka 2012, 2013 na 2015.

Cameroon nao wamejikakamua vyema kuweza kufika fainali.

Miongoni mwa kikosi cha Cameroon ni wachezaji wanaosakata soka Uingezea Arnaud Djoum na Clinton N'Jie,

Misri nayo ina wachezaji watatu kutoka Ligi kuu ya Uingerza wakiwemo Ahmed Elmohamady (Hull) Mohamed Elneny (Arsenal) and Ramadan Sobhi (Stoke)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cameroon na Misri wameshinda kombe la Afcom mara 11

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea