Schemeichel: Leicester huenda ikashushwa daraja

Kipa wa Leicester City Schmeichel
Image caption Kipa wa Leicester City Schmeichel

Kipa wa klabu ya Leicester Kasper Schmeichel amesema kuwa timu hiyo huenda ikashushwa daraja iwapo itaendelea kupoteza mechi zake.

The Foxes wako pointi moja juu ya timu zilizopo katika orodha ya timu zitakazoshushwa daraja baada ya kushindwa 3-0 nyumbani na Manchester United.

Leicester haijashinda mechi hata moja mwaka huu 2017 na hawajafunga hata bao moja katika mechi tano ilizocheza.

''Sisi ndio bingwa mtetezi lakini kusema kweli ni matatizo'', alisema Schmeichel.Kila mchezaji anakerwa.Sio hali nzuri.ni wakati wa kila mmoja wetu kujikukuta na kusimama kidete la sivyo tushushwe daraja''

Wakati kama huu mwaka uliopita, Leicester ilishinda 3-1 katika uwanja wa Etihad dhidi ya Manchester City na kupanda juu ya jedwali wakiwa na pointi tano kabla ya kushinda taji la ligi.

Sasa wako pointi 38 nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea huku ripoti zikisema kuwa mkufunzi Claudio Ranieri hapendwi tena na wachezaji wake.