Nyota wa Rugby Joost van der West-huizen amefariki Dunia

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nyota wa Rugby ,Marehemu Joost van der West-huizen

Mchezaji wa zamani wa Afrika Kusini na Nahodha wa timu ya taifa ya mchezo wa Rugby Joost van der West-huizen amefariki akiwa na miaka 45, kwa ugonjwa wa motor neurone.

Alikuwa nahodha wa Springboks kwa miaka minne, Van der West-huizen alishinda Kombe la Dunia mwaka 1995 pia katika michezo ya kimataifa ya mwaka 1993 ,2003 na mwaka 1999 katika Kombe la Dunia, kabla ya kustaafu kwake mwaka 2003.

Van der West-huizen amepatwa na umauti akiwa hospitali mjini Johannesburg siku ya Jumamosi.