Bondia Mohamed Matumla-afanyiwa upasuaji wa kichwa

Haki miliki ya picha Google
Image caption Bondia Mohamed Matumla

Bondia wa Tanzania Mohamed Matumla amefanyiwa upasuaji wa kichwa kutokana na maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa na Bondia Mfaume mfaume katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika katika ukumbi wa Ndani wa taifa jijini Dar es salaam.

Mwandaaji wa pambano hilo Jocktan Masai amaesithibitisha kuhusina na tukio hilo lililotokea katika pambano lilsilo la Ubingwa,anasema Matumla alipatwa na mkasa huyo katika raundi ya saba ya pambano.

Bondia huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospatali ya taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam .