Barcelona yatinga fainali kombe la mfalme

Image caption Barcelona wakishangilia ushindi

Timu ya soka ya Barcelona imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la mfalme au copa De rey nchini Hispania kufuatia sare ya kufungana goli 1-1 na Atletico Madridi.

Goli la Barcelona limefungwa na Luiz Suarez huku lile la Atletico Madrid likifungwa na Kevin Gameiro.

Kwa matokeo hayo Barcelona wanasonga mbele kwa faida ya magoli matatu dhidi ya mawili ya Atletico Madrid na hivyo wakitaraji kukutana kati ya Alaves or Celta Vigo katika mchezo wa Fainali.

Katika mchezo huo mchezaji Luiz suarez alitolewa kwa kadi nyekudu baada ya kuwa na kadi mbili za njano .