El-Hadj Diouf awazodoa wacameroon

Haki miliki ya picha Google
Image caption El-Hadj Diouf, Nguli wa zamani wa soka wa kimataifa wa SenegaL

Nguli wa zamani wa soka wa kimataifa wa Senegal, El-Hadj Diouf amesema wachezaji nane wa Cameroon waliokataa wito wa kuichezea timu yao ya taifa katika michuano ya Mataifa ya Afrika watajutia uamuzi huo maisha yao yote.

Nyota kadhaa wa Cameroon akiwemo Joe Matip anayekipiga Liverpool, Eric Choupo-Moting na Allan Nyom wote wakicheza Schalke walikataa kuitumikia nchi yao kwa madai binafsi haswa suala la kuchelewa kwa posho zao.

Diouf amesema haelewi watu wanaoikataa nchi yao kwa siku zote mtu anayekataa kwao, hafahamu atapokwenda amsema

Diouf amesema siku zote ni ngumu kuwa Muafrika kwani hata kama ukiwa kocha mzuri namna gani lakini hawataweza kukupa klabu kama Barcelona, Paris Saint-Germain, Liverpool au Manchester United uzifundishe.