Wigan , Norwich hakuna mbabe -championship

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wigan Athletic na Norwich city wakichuana

Michuano ya championship ya kufuzu kutinga Ligi kuu ya England imeendelea hapo jana jumanne kwa mchezo mmoja ambao ulizikutanisha timu za Wigan Athletics na Norwich city.

Mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kugawana alama kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.

Norwich city ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao dakika ya 40 kipindi cha kwanza kupitia kwa Nelson Oliveira,na baadaye Wigan wakasawazisha bao hilo na kuongeza bao la pili kupitia kwa Omar Bolge dakika ya 62,68 kipindi cha pili.

Norwich wakasawazisha bao la pili kupitia kwa Mitchell Djiks.

Michuano hiyo itaendelea tena siku ya ijumaa tarehe 10 februali kwa mchezo mmoja Sheffield Wednesday itaivaa Birmingham City.