Leicester City wasonga Kombe la FA

Haki miliki ya picha Google
Image caption Leicester city na Derby County wakichuana

Klabu ya soka ya Leiceister city hatimaye imeweza kulinda heshima katika uwanja wake wa nyumbani wa King Power kufuatia ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Derby County katika michuano ya mwaka huu ya FA CUP ukiwa ni mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kutinga Raundi ya 5 ya michuano hiyo.

Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizi tayari zilikuwa zimefungana bao 1-1 na kulazimika kuongezwa muda wa ziada.

Leicester city ndio walikuwa wa kwanza kuandikisha bao kupitia kwa Andy King, na baadaye Derby County wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Abdoul Camara, huku Onyinye Wilfredy Ndindi akiongeza bao la pili kwa upande wa Leceister city katika dakika ya 94 muda wa nyongeza.

Dakika ya 114 Demaria Gray akapigilia msumari wa mwisho katika jeneza la Derby County kwa kuandika bao la tatu na la mwisho.

Kwa matokeo hayo sasa Leicester city watakutana na Milwall katika raundi ya tano wakiwa ugenini.