Woods na changamoto za majeraha

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tiger Woods

Mshindi wa mara kumi na nne wa mchezo wa Golf Tiger Woods ameasema kamwe yeye hataendelea kujiona ni mchezaji mkubwa kwa sababu ya kukabiliwa na idadi kubwa ya majeruhi katika fani yake.

Woods mwenye miaka 41, alitupwa nje ya mashindano ya Dubai Desert Classic kabla ya duru ya pili ya mwezi huu kwa sababu ya maumivu, alitarajia kurejea tena dimbani mwezi wa kumi na mbili baada ya kufanyiwa upasuaji

Ameviambia vyombo vya habaei vya Dubai kuwa kwa muda mwingi kuwa kumekuwa na changamoto nyingi hakuweza kufikiria kuerejea tena na ilikuwa ni vigumu

Na kwa sasa Ana matumaini ya kushindana katika michuano ya Masters kuanzia mwezi April .