Nyom asema hajutii kutoichezea Cameroon

Cameroon Haki miliki ya picha Google
Image caption Mlinzi wa klabu ya West Brom, Allan Nyom

Mlinzi wa klabu ya West Brom, Allan Nyom amesema hajutii kutoenda kuichezea timu yake ya taifa ya Cameroon katika michuano ya kombe la mataifa Afrika nchini Gaboon na kubaki na klabu yake ya West Brom.

Licha ya baadhi ya wachezaji wa Cameroon kushindwa kwenda kuitumikia timu yao ya taifa ,Cameroon ilifanikiwa kutwaa taji baada ya kuifunga Misri katika mchezo wa afainali na kuafanikiwa kubeba taji

Nyom alikuwa miongoni mwa wachezaji kadhaa walikataa kwenda kuichezea nchi yao kwenye michuano hiyo nchini Gabon wakiwemo wachezaji Wengine ikiwa ni pamoja na Joel Matip anayeichezea Liverpool nchini England.

Pamoja na hayo kocha wa Cameroon Hugo Broos amesema hajutiii uamuzi Nyom wa kutokwenda kuichezea Cameoon katika michuano ya kimataifa.

West Brom inashika nafsi ta sita katika msimamo wa Ligi Kuu ya England na Jumamosi watakuwa wageni wa West Ham Uwanja wa London.