Dimitri Payet na Memphis Depay wafunga mabao Ufaransa

Dimitri Payet Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dimitri Payet alirejea Marseille akitokea West Ham kwa £25m Januari

Dimitri Payet na Memphis Depay wamefunga mabao yao ya kwanza katika klabu za Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1, tangu walipohama klabu zao za Uingereza Januari.

Payet, ambaye alitoka West Ham, alifunga kutokana na frikiki na kusaidia Marseille kuwalaza Guingamp 2-0.

Mchezaji aliyetoka Manchester United Depay aliingia kama nguvu mpya kipindi cha pili na kuwafungia Lyon bao la nne na kuwawezesha kulaza Nancy 4-0.

Mholanzi huyo pia ndiye aliyeshindia Lyon penalti iliyowawezesha kufunga bao la tatu.

Kwingineko, Nice walizidi kuwawekea presha viongozi wa ligi Monaco kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya St Etienne.

Wamo na alama 52, nafasi moja nyuma ya mabingwa watetezi Paris St-Germain kwa wingi wa mabao.

Klabu zote mbili hata hivyo zimeachwa nyuma na Monaco kwa alama tatu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Memphis Depay alikaa msimu mmoja unusu Manchester United kabla ya kuhamia Lyon kwa £16m

Mada zinazohusiana