Alves kuivaa Barcelona -Copa De Rey

Haki miliki ya picha Google
Image caption Copa De Rey

Katika Michuano ya Copa De Rey - Klabu ya Alves ya Nchini Hispania inatarajia kumenyana na Timu kongwe ya Barcelona katika mchezo wa Fainali ya michuano ya hiyo baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Celta Vigo.

Edgar Mendez alifanikiwa kuipeleka timu yake katika hatua hiyo ya Alves BAO pekee la Dakika ya 81 la ya soka ya Fainali ya Kombe la Mfalme wa Spain, Copa del Rey, ambako watakutana na Mabingwa Watetezi Barcelona, baada ya kuwabwaga Celta Vigo 1-0.

Ushindi huo uliopatikana Nyumbani kwa Alaves, Mendizorrotza, ulileta shamrashamra kubwa na umewaingiza Fainali kuwania kubeba Kombe hili kwa mara ya kwanza.

Hii ni Fainali ya Kwanza kwa Alaves tangu 2001 walipofungwa 2-1 na Liverpool kwenye UEFA CUP.

Juzi, Barcelona walitinga Fainali ya Copa del Rey kwa kuitoa Atletico Madrid Jumla ya Bao 3-2 kwa Mechi 2 baada ya kushinda ya kwanza 2-1 na kutoka 1-1 katika Mechi ya Pili.

Alves, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu na kutinga La Liga, ni mwiba kwa Barca kwani Septemba huko Nou Camp iliipiga Barca 2-1.

Fainali ya Copa del Rey ni Mei 27 na Mshindi wake atatinga hatua ya Makundi ya UEFA EUROPA LIGI hapo Mwakani.